Monday, June 4, 2012

MBEYA UPDATE: WAKAZI 1800 HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA MBARALI



W
akazi 18,333  Wilayani Mbarali mkoani Mbeya hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu hali inayozua changamoto kwa serikali na wadau wengine kuwabadilisha wakazi hao ili watambue umuhimu wa elimu kwa watoto wao.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Kened Ndingo uwepo wa idadi kubwa ya wananchi wasiojua kusoma,kuandika na kuhesabu unachangia kuwepo kwa uelewa duni juu ya umuhimu wa elimu wilayani humo

Ndingo ameyasema hayo  katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa kanisa la Lutherani katika mji mdogo wa Rujewa na kufafanua kuwa pamoja na juhudi kubwa inayofanywa na serikali kuhakikisha kila mtoto aanapata elimu stahili,uthamani wa elimu kwa wakazi wa wilaya hiyo unaonekana kushuka siku hadi siku.

Amesema tofauti na maeneo mengine ambako wakazi wanakimbilia elimu kwa kuhakikisha waanawawezesha watoto wao kuipata,wakazi wilayani kwake hawaoni umuhimu huo na imefika waakati sasa hawajali elimu hata kwa watoto wao.

Kwa upande wake ofisa elimu shule za msingi Wilayani humo Rustika Turuka amesema Wilaya imekuwa ikishika kati ya nafasi ya 6 na 8 ya ufaulu kimkoa kati ya wilaya 8 zilizopo mkoani Mbeya katika matokeo ya darasa la saba.

Naye mmoja wa wadau waliohudhuria kikao hicho Ophia Nzobonaliba  amesema tatizo kubwa lipo kwa jamii za wafugaji ambao wamekluwa wakiona bora watoe fidia kwa kutopeleka watoto wao shule na kuwaacha waendelee kuchunga mifugo yao.

Imeandikwa na Joachim Nyambo, Mbeya

No comments:

Post a Comment