Sunday, April 8, 2012

VIDIC NJE MSIMU ULIOBAKIA.

MENEJA wa timu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema kuwa beki wa timu hiyo Nemanja Vidic atakuwa tayari kucheza msimu ujao wa 2012-2013. Ferguson amesema kwamba beki huyo wa kati raia wa Serbia lazima apate muda kuliko kumharakisha kurejea uwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti, unaomfanya akose mechi zote zilizobaki za United za kujianda na msimu mpya pia. Wakati kocha huyo raia Scotland anahisi nahodha wake atakosa mechi za mwanzoni za msimu, kuna alama za kujiuliza kuhusu kiwango cha safu ya ulinzi hivi sasa. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa atawatumia wachezaji Phil Jones na Chris Smalling ambao walinunuliwa kwa mikataba mirefu kwani wanaonyesha wanaweza kucheza nafasi nyingine mpaka hapo Vidic atarejea na kukamilisha safu ya ulinzi wa klabu hiyo. Aliongeza pia Vidic hatajumuishwa katika ziara ya kikosi hicho kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Uingereza lakini atakuwa tayari kucheza mechi za mwanzoni mwa msimu ujao wa ligi.

No comments:

Post a Comment