Sunday, April 8, 2012

TERRY AKIRI WANAE KUMHUSUDU MESSI.

NAHODHA wa Chelsea John Terry amekiri kuwa anaweza kusababisha mgawanyiko katika familia yake wakati timu yake hiyo itapopambana na Barcelona katika mchezo wa nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kauli hiyo ya Terry imekuja kutokana na wanae wawili mapacha kumhusudu kupindukia mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na amekuwa kama kioo chao kuliko baba yao. Sasa watoto hao wa Terry itabidi wachague nani wa kumuunga mkono wakati timu hizo zitapokutana katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo na nahodha huyo anajua hatari atayopata wakati akirudi nyumbani kama atamkwatua Messi katika mchezo huo. Terry amesema kuwa watoto wake hao wanamhusudu Messi na wote wana fulana za timu ya Barcelona zenye jina la mchezaji huyo mgongoni na walipenda kipindi nilichobadilishana fulana na mchezaji huyo wakati timu hizo zilipokutana huko nyuma.

No comments:

Post a Comment