Thursday, April 12, 2012

MESSI NI BORA KULIKO MARADONA-ARDILES.

Ossie Ardiles.
NYOTA wa zamani wa Argentina Ossie Ardiles amesema kuwa Lionel Messi ni bora kuliko mchezaji mwenzake wa zamani Diego Maradona pamoja ana kwamba nyota huyo wa Barcelona bado hajaonyesha cheche zake katika timu ya taifa ya nchi hiyo. Akihojiwa na waandishi wa habari nchini kwao Ardiles amesema kuwa amecheza na Maradona kwa miaka saba ni mchezaji mkubwa na sikudhania kama anaweza kutokea mchezaji wa aina yake lakini analazimika kusema kuwa Messi ni zaidi yake. Ardiles anaamini kuwa Messi anaweza kuisaidia Argentina kushinda Kombe la Dunia kabla hajastaafu kucheza soka. Maradona alikuwa nahodha wa Argentina wakati nchi hiyo iliponyakuwa Kombe la Dunia mwaka 1986 na pia aliiongoza nchi hiyo katika michuano ya mwaka 1990 ambapo walifika fainali. Messi amekuwepo katika kikosi cha Argentina katika michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2006 na 2010 ambapo timu hiyo imekuwa ikitolewa katika hatua ya robo fainali.

No comments:

Post a Comment