Thursday, April 12, 2012

BRAZIL HAS FOCUS ON OLYMPIC TOURNAMENT.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Brazil Jose Maria Marin amesema kuwa shirikisho hilo linaelekeza nguvu zake kuhakikisha timu ya taifa ya nchi hiyo inashinda medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini London, Uingereza baadae mwaka huu. Michuano ya Olimpiki ni michuano pekee ambayo mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia bado hawajashinda. Marin amesema kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanabakisha Kombe la Dunia katika ardhi yao ya nyumbani mwaka 2014, lakini kwa mwaka huu watasahau hilo kwa muda na kuhakikisha wananyakuwa medali ya dhahabu katika michuano hiyo. Aliendelea kusema kuwa Olimpiki ni taji pekee ambalo Brazil haijashinda hivyo atahakikisha anaisaidia kwa lolote kuhakikisha kikosi chao kinapata maandalizi ya kutosha kabla ya kuanza kwa michuano hiyo. Brazil imefanikiwa kushinda medali ya fedha katika michuano ya Olimpiki mwaka 1984 na 1988, ambapo pia walifanikiwa kuchukua medali ya shaba mwaka 1996 na 2008 wakati kikosi hicho kikiongozwa na Ronaldinho ambaye alikuwa mchezaji bora wa dunia mara mbili kwa wakati huo.

No comments:

Post a Comment