Thursday, April 12, 2012

HAVELANGE ATOLEWA ICU.

Daktari anayemtibu Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Joao Havelange amesema hali yake inaendelea vyema na sasa anapumua bila kutumia mashine kama ilivyokuwa hapo awali. Daktari huyo aitwae Joao Mansur Filho wa hospitali ya Samaritano iliyopo jijini Rio de Janeiro amesema kuwa Havelange ambaye ana umri wa miaka 95 ametolewa katika wodi ya wagonjwa mahututi na sasa amelazwa wodi ya wagonjwa wa kawaida. Havelange alipatwa na tatizo la kushindwa kupumua Jumatatu wakati akiwa hospitalini hapo wakati akitibiwa maambukizi aliyopata katika kifundo chake cha mguu lakini Filho aliongeza kuwa hajui lini watamruhusu mzee huyo kurudi nyumbani kwake. Havelange ambaye aliwahi kuwa rais wa FIFA kuanzia mwaka 1974 mpaka 1998 alilazwa hospitalini hapo mwezi uliopita kutokana na maambukizi aliyopata katika kifundo chake cha mguu.

No comments:

Post a Comment