Thursday, April 12, 2012

MARIN AMWANGUKIA ROMARIO.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Brazil, Jose Maria Marin amemuomba mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo Romario kusadia katika maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 pamoja na nyota huyo kukosoa maandalizi yanayofanywa na nchi hiyo. Akikaririwa jana Marin amesema kuwa nyota huyo wa zamani ambaye kwa sasa ni mbunge mchango wake katika maandalizi hayo utakuwa ni muhimu. Marin ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo aliendelea kusema kuwa Romario pamoja na wachezaji wengine nyota ambao wamewahi kuitumikia nchi hiyo wakiungana kwa pamoja basi hapana shaka wataandaa Kombe la Dunia ambalo haliwezi kusahaulika. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya nchi hiyo ambavyo vilimkariri Romario akisema kuwa anafurahishwa na uongozi wa Marin na atajaribu kusaidia katika maandalizi hayo kadiri awezavyo.

No comments:

Post a Comment