Thursday, April 12, 2012

ABIDAL AENDELEA VYEMA.

RAIS wa klabu ya Barcelona Sandro Rosell amesema kuwa beki wa klabu hiyo Eric Abidal anendelea vizuri baada ya siku moja ya kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha ini. Rosell amesema kuwa Abidal pamoja na mpwa wake ambaye alijitolea kumpa sehemu ya ini lake wote wanaendelea vizuri ingawa alishindwa kuelezea kwa undani zaidi kutokana na maombi ya familia yake.  Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 32, alifanyiwa upasuaji huo wa kupandikizwa sehemu ya ini ambalo alipewa na mpwa wake aitwae Gerard zoezi ambalo lilichukua muda wa masaa tisa katika hospitali moja iliyopo jijini Barcelona. Katika taarifa iliyotolewa na gazeti moja jijini humo limesema kuwa upasuaji wa mchezaji huyo ulianza saa tisa za jioni kwa saa za huko na kumalizika saa sita za usiku.

No comments:

Post a Comment