Monday, April 9, 2012

DANI ALVES KUIKOSA GETAFE.

MENEJA wa Barcelona Pep Guardiola anatakiwa kuipanga safu yake ya ulinzi upya katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania dhidi ya Getafe kutokana uwezekano mkubwa wa kumkosa beki machachari wa timu hiyo Dani Alves kutokana na majeraha. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alipata majeraha hayo katika mchezo ambao timu hiyo iliifunga Real Zaragoza mabao 4-1 Jumamosi iliyopita ambapo alilazimika kutolewa nje dakika ya 68 ya mchezo huo. Baada ya kufanyiwa vipimo kadhaa jana baada ya kupata majeraha hayo timu hiyo ilithibitisha katika mtandao wao kuwa mchezaji huyo ameumia misuli katika paja lake la kushoto. Haijathibitishwa ni muda gani mchezaji huyo ambaye pia amewahi kuichezea klabu ya Sevilla atakuwa nje ya uwanja lakini inavyoonekana ataukosa mchezo dhidi ya Getafe. Nafasi ya Beki huyo inatarajiwa kuzibwa na Martin Montoya kesho ambapo pia kijana huyo ndio alieingia kuchukua nafasi yake katika mchezo dhidi ya Zaragoza.

No comments:

Post a Comment