Monday, April 9, 2012

BARCELONA WANAFUNGIKA-ESSIEN.

KIUNGO wa Chelsea Michael Essien anaamini kuwa timu ya Barcelona inafungika na anahisi wakati wa klabu yake hiyo kunyakuwa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza umewadia. Klabu hiyo inayotoka Magharibi mwa jiji la London inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Barcelona katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya michuano hiyo utakaochezwa April 18 mwaka huu na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana anaamini Chelsea itaifunga timu hiyo. Essien amesema kuwa wameshacheza na klabu hiyo mara chache katika kipindi cha miaka nane au zaidi na wanafungika hivyo anadhani ni wakati wa Chelsea kuwavua ubingwa Barcelona ambao wanautetea. Kiungo huyo mzaliwa wa Accra alikuwa na wakati mgumu msimu huu na klabu yake hiyo akiwa amecheza michezo 14 katika msimu kutokana na majeraha yanayomsumbua kwa kipindi kirefu.

No comments:

Post a Comment