Monday, April 9, 2012

PELE APIGIA CHAPUO KOCHA MZAWA KUINOA BLACK STARS.

Abedi Pele
NGULI wa soka wa zamani nchini Ghana, Abedi Pele ameeleza kuwa hakuna tatizo lolote kama Shirikisho la Soka la nchi hiyo-GFA litateua kocha mzalendo kwa ajili ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa. Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo iliyopo Magharibi mwa bara la Afrika amesema kuwa kocha mzalendo anaweza kuwa na uwezo sawa na kocha kutoka nje na muda mwingine bora zaidi. Aliendelea kusema kuwa sio jambo la busara kutupilia mbali suala la kuteua kocha mzalendo kukinoa kikosi hicho kwani mataji yote ambayo timu hiyo imeshinda walishinda wakiwa wananolewa na makocha wazawa ambao ni mkongwe C.K Gyamfi ambaye alikiwezesha kikosi hicho kushinda Kombe la Afrika mara tatu na Fred Osam-Doudu ambaye yeye alinyakuwa taji hilo mara moja. Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa ambaye ni mzaliwa wa Ghana, Marcel Desailly amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya kocha aliyetimuliwa Goran Stevanovic ambapo Pele anasema kuwa halitakuwa chaguo baya kama wakimteua. Shirikisho hilo linatarajiwa kumtaja kocha mpya wiki hii.

No comments:

Post a Comment