Wednesday, April 11, 2012

TANZANIA YAZIDI KUPOROMOKA VIWANGO VYA FIFA.

TANZANIA imeendelea kuporomoka katika viwango vya ubora wa soka duniani baada ya kushuka kwa nafasi nne katika orodha mpya iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Kabla ya kutolewa kwa orodha hiyo mpya Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya 141 ambapo sasa imeporomoka mpaka nafasi ya 145 katika msimamo wa orodha hizo. Katika nchi za Afrika Ivory Coast ndio imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Ghana, Algeria Mali na mabingwa wa Afrika Zambia huku nchi za Gabon, Libya, Misri, Tunisia na Nigeria zikikamiliza kumi bora ya timu za Afrika. Hispania bado imeendelea kuongoza orodha hiyo huku Uholanzi ambao walikuwa wakishika nafasi ya pili wakiporomoka mpaka nafasi ya nne nyuma ya Ujerumani na Uruguay huku ureno ikipanda mpaka nafasi ya tano ikifuatiwa na Brazil, Uingereza, Croatia, Denmark na Argentina.

No comments:

Post a Comment