Wednesday, April 11, 2012

FIFA RULES IN FAVOUR OF TP MAZEMBE IN CAF CHAMPIONS LEAGUE DISPUTE.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA kupitia Kamati yake ya usuluhishi wa migogoro imetoa uamuzi wa kuunga mkono rufani ya klabu ya TP Mazembe kufuatia kutolewa kwao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika kwasababu za kumchezesha mchezaji ambaye hakustahili. Uongozi wa klabu hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC ulitangaza maamuzi hayo ya FIFA na kuahidi kuwa watachukua hatua zinazostahili kwa ajili ukarabati wa jumla wa klabu hiyo. Msemaji wa klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Lubumbashi, amesema kuwa waligundua maamuzi yaliyotolewa na kamati ya FIFA siku moja iliyopita kitu ambacho kinawapa ushindi wa kesi yao waliyoifungua dhidi ya FIFA kuhusiana na suala la kutolewa kwao. Mazembe ilitolewa katika michuano hiyo mwaka jana baada ya klabu ya WAC Casablanca ya Morocco kutuma rufani Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF kwa kumchezesha beki Janvier Besala Bokungu ambaye walidai bado alikuwa na mkataba na klabu ya Esperance ya Tunisia. Mazembe ambao walishika nafasi ya pili katika michuano ya klabu bingwa ya ya dunia mwaka 2010 walishindwa kuleta vithibitisho kwa CAF kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 23 alikuwa ameshamaliza mkataba wake na Esperance kabla ya kutua jijini Lubumbashi na hivyo kupea adhabu hiyo.

No comments:

Post a Comment