4 Juni mwaka 1989, wanafunzi kadhaa wa vyuo vikuu vya China waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa na polisi katika mji mkuu wa nchi hiyo Beijing.
Siku hiyo maelefu ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya China walikuwa wamejikusanya katika mzunguko wa Tiananmen mjini Beijing, wenye maana ya 'Amani ya Mbinguni" wakitaka kuwepo mazingira ya wazi ya kisiasa nchini humo, kupunguzwa uwezo wa chama cha kisoshalisti, kuongezwa uwezo wa bunge na kuchaguliwa wawakilishi wake. Ingawa serikali ya China ilipinga maandamano hayo lakini wanafunzi waliendela kukusanyika na mwishowe askari polisi na vikosi vya jeshi kutumia silaha kuwakandamiza wanafunzi hao waliokuwa wakiandamana ambapo baadhi waliuawa na kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment