Dirk Kuyt amejiunga na magwiji wa soka wa Uturuki Fenerbahce kutoka Liverpool kwa mkataba wa miaka 3.
Mdachi huyo alihamia Anfield kutoka Feyenoord mwaka 2006 na kucheza mechi 207 akiwa na The Reds.
Lakini mshambuliaji huyo mwenye miaka 31alianza msimu uliopita akiwa analikalia benchi chini ya Kenny Dalglish na sasa ameamua kuondoka Anfield siku chache baada ya Brendan Rodgers kutajwa kama kocha mpya wa Liverpool. Akiwaaga mashabiki Kuyt alisema: "Klabu na mashabiki siku zote mtakuwa kwenye moyo wangu. Kuchaguliwa kwa kocha mpya hakuchangia kuondoka kwangu.
"Wakati Fenerbahce waliponifuata na kuniambia mipango yao, tangu wakati huo nilishahama Liverpool. Walinipa hali ya kujiamini ambayo nilishaipoteza."

No comments:
Post a Comment