Rais Joyce Banda wa Malawi ameihakikishia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kuwa serikali yake itamkamata Rais Omar Al-Bashir wa Sudan endapo atatia miguu yake nchini humo.
Rais Banda ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na Andrew Mitchell, waziri wa Uingereza anayehusika na masuala ya kimataifa ambaye yuko Malawi kwa ziara ya kikazi. Msimamo huo wa Joyce Banda unatofautiana na ule wa mtangulizi wake, hayati Bingu wa Mutharika ambaye alimruhusu Rais Bashir kuitembelea hiyo mwaka uliopita licha ya waranti wa ICC dhidi ya kiongozi huyo wa Sudan. Umoja wa Afrika AU umekosoa msimamo huo wa Rais Banda na umemtaka kiongozi huyo kubadili msimamo wake ili kumruhusu Rais Bashir kuhudhuria mkutano wa 19 wa viongozi wa AU mwezi ujao mjini Blantyre.
No comments:
Post a Comment