Sunday, April 8, 2012

RONALDINHO KUITEMA FLAMENGO.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Flamengo Ronaldinho Gaucho amedokeza kuwa anaweza kuondoka klabuni hapo lakini amesema kuwa kama kweli ataondoka basi atafuata taratibu zote za uhamisho. Nyota huyo wa zamani wa Barcelona na AC Milan alifunga bao la ushindi wakati timu yake ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Vasco da Gama Jumamosi lakini mustakari wa mchezaji huyo msimu huu umekuwa na utata. Ronaldinho amesema kuwa toka alipowasili katika kllabu hiyo amekuwa akicheza kwa kujitua na upendo mkubwa na hivyo ndivyo alivyokuwa akihitaji kufanya kila analoweza kuisaidia klabu hiyo lakini alidokeza kuwa anaweza kuihama klabu hiyo yenye maskani yake jijini Rio de Janeiro. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alijiunga na klabu hiyo Januari mwaka 2011 na ana mkataba utakaoisha mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment