Sunday, April 8, 2012

PSG BADO YAONYESHA NIA KWA KAKA.

MENEJA wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG ya Ufaransa Carlo Ancelotti kwa mara nyingine ameonyesha nia yake ya kumnyakua kiungi wa Real Madrid Kaka ingawa amekuwa hana uhakika kama mchezaji huyo atakuwa sokoni katika kipindi kijacho cha majira ya kiangazi. Klabu hiyo imekuwa ikimfukuzia mchezaji huyo katika kpindi cha nyuma na Ancelotti alikiri Februari mwaka huu kwamba kama mchezaji akiwekwa sokoni basi ataweza kumnunua. Bado mpaka sasa haijajulikana kama kocha wa Madrid Jose Mourinho atamjumuisha katika mipango yake ya baadae mchezaji huo ambaye katika miezi ya hivi karibuni ameonekana kurudisha makali yake, lakini Ancelotti ameweka wazi kuwa anataka kufanya kazi na mchezaji huyo ambaye alikuwa nae wakati alipokuwa akikinoa kikosi cha AC Milan. PSG inatarajiwa kuifuata Olympique Marseille leo wakiwa na matumaini ya kushinda mchezo huo ili kukamata usukkani wa Ligi Kuu ya nchi hiyo wakati Kaka anatarajiwa kuwemo katika kikosi chake kitachopambana na Valencia baadae leo.

No comments:

Post a Comment