Wednesday, April 11, 2012

BRAD JONES THANKS LIVER FANS FOR THE SUPPORT SINCE HIS SON DEATH.

GOLIKIPA wa Liverpool Brad Jones ameutoa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Blackburn Rovers kwa mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa pamoja nae wakati alipofiwa na mwane wa kiume. Katika mchezo huo Jones ambaye aliingia akitokea benchi la wachezaji wa akiba alifanikiwa kuokoa mkwaju mmoja wa penati na kufungwa mwingine mmoja hivyo kuiwezesha timu hiyo kuibuka kidedea katika mchezo huo. Jones alifiwa na mtoto wake wa kiume aitwae Luca ambaye alifariki kwa kansa ya damu au lugha ya kitaalamu Leukemia, Novemba mwaka jana ambapo wiki iliyopita mke wake alijifungua mtoto mwingine aliyemwita Nico. Akiongea mara baada ya mchezo huo Jones amesema kuwa ilikuwa ni miezi migumu toka alipofiwa na mwanae huyo lakini yeye, mkewe na mtoto wao Nico ambaye wamemzaa hivi karibuni waliwashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwa pamoja nao katika kipindi hicho kigumu. Mchezaji wa kimataifa wa Australia mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni golikipa namba tatu wa timu hiyo aliingia akitokea benchi dakika ya 26 baada ya golikipa Alexander Doni aliyechukua nafasi ya Pepe Reina kutolewa nje kutokana na kumchezea vibaya Junior Hoilett.

No comments:

Post a Comment