Tuesday, April 10, 2012

BALOTELLI AMWANGUKIA MANCINI.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Mario Balotelli ameomba radhi mjini Milan kwa utovu wake wa nidhamu na kuomba asiondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Italia kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya. Mchezaji huyo alipewa kadi nyekundu ya nne katika misimu miwili akiwa na City ambapo timu yake iiilala kwa bao 1-0 mbele ya Arsenal Jumapili, jambo ambalo limeibua swali, huenda Balotelli amevunja agizo la nidhamu na uadilifu lililowekwa na kocha wa Italia, Cesare Prandelli. Balotelli aliomba radhi kwa kitendo alichofanya ambacho kiliigharimu timu yake na pia alimuomba radhi kocha wake Roberto Mancini ambaye alidai anampenda na kumtakia mema ingawa alidai alicheza faulo hizo sio kwa ugomvi bali ni kwa matukio ya mchezo. Balotelli alipewa kadi nyekundu dakika ya 90, baada ya kupewa kadi ya kwanza ya njano kwa kumchezea rafu Bacary Sagna, dakika tatu baada ya Mikel Arteta kuifungia Arsenal.

No comments:

Post a Comment