Wednesday, April 11, 2012

ABIDAL UNDERGOES LIVER TRANSPLANT.

BEKI wa klabu ya Barcelona amefanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini jingine jana ambapo zaidi ya mashabiki 70,000 waliohudhuria mchezo dhidi ya Getafe jana wakati timu hiyo iliposhinda mabao 4-0 walikuwa wamevaa fulana zenye jina la mchezaji huyo ili kuonyesha kwamba wapo pamoja nae katika kipindi hicho kigumu. Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo Andoni Zubizarreta amesema kuwa mchezaji huyo alikuwa katika chumba cha upasuaji wakati mchezo huo ulipokuwa ukiendelea ambapo mashabiki 76,041 waliohudhuria mchezo huo walivaa jezi zenye namba anayovaa Abidal. Zubizarreta amesema kuwa kwa muda ule hawakuwa na taarifa yoyote lakini walitegemea madaktari watawahabalisha lolote linaloendelea kwakuwa wanaamini yuko katika mikono salama hospitalini hapo. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 32 alifanyiwa upasuaji wa ini kuondoa uvimbe uliokuwepo Machi mwaka 2011 na alifanikiwa kurejea uwanjani kumalizia msimu uliobakia ambapo alicheza mpaka mwezi uliopita kabla ya klabu hiyo kusema kwamba upasuaji wa kupandikiza ini jingine ni lazima kwa mchezaji huyo. Kocha wa Barcelona akihojiwa mara baada ya mchezo dhidi ya Getafe amesema kuwa ushindi ambao timu yake waliupata ni kwa ajili ya Abidal pamoja na binamu yake ambaye amejitolea kumpa ini mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment