skip to main |
skip to sidebar
2013 AFCON CITIES TO BE NAMED SOON.
|
Mvuzo Mbebe |
KAMATI ya Maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 inatarajia kutangaza miji itakayokuwa wenyeji wa michuano hiyo mwishoni mwa mwezi huu. Ofisa Mkuu wa kamati hiyo Mvuzo Mbebe alithibitisha hilo wakati akiongeza na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vikitaka ufafanuzi kuhusiana na ucheleweshwaji wa kutaja miji ambayo itakuwa wenyeji wa michuano hiyo. Mbebe alifafanua kuwa ucheleweshwaji huo unafanywa na serikali ya nchi hiyo ambao wanadai kuwa wana taratibu zao inabidi wapitie ndio waruhusu kamati hiyo kuendelea na kazi yake. Mbebe alizungumza hayo wakati akiwa jijini Johannesburg ambapo Chama cha Soka cha nchi hiyo-SAFA kilikuwa kinatiliana saini ya makubaliano ya maandalizi ya michuano hiyo na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF.
No comments:
Post a Comment