Tuesday, June 5, 2012

TANZANIA FOOTBALL NEWS: TAIFA STARS YAJIPANGA DHIDI YA GAMBIA JUNI 10


WAKATI kikosi cha timu  ya Taifa 'Taifa Stars' kikirejea jijini asubuhi ya leo kutoka Ivory Coast, kocha mkuu wa timu hiyo Mdenish Kim Poulsen ameweka wazi kuisaka mikanda ya timu ya Taifa ya Gambia ili kuweza kuifanyia kazi.

Stars na Gambia zitakwaana juni 10 katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya mchujo ya kombe la Dunia. Kikosi cha Stars ambacho kilikuwa nchini Ivory Coast  ambapo kilifungwa mabao 2-0 katika mchezo wa kuwania kampeni hizo uliopigwa jumamosi iliyopita.

Stars imeingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo na Gambia

No comments:

Post a Comment