Tuesday, June 5, 2012

TANZANIA FOOTBALL NEWS: SIMBA KUSAJILI WAWILI KUTOKA DYNAMOS


 MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba wapo mbioni kusajili nyota wawili kutoka klabu ya Power Dynamos ya Zambia, imefahamika. 
MMoja ya viongozi wa Simba aliliambia Tanzania Daima kwamba mbali na Zambia pia wana mpango wa kusajili mchezaji mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). 

Alisema usajili wao utalenga nafasi ya beki na mshambuliaji ambapo watasajili nyota hao wa Zambia kuziba nafasi ya Juma Nyoso ambaye  kwa sasa hana nafasi tena katika kikosi cha timu yao. 

“Pia kutoka huko huko Power Dynamos huenda tukasajili mshambuliaji mwingine…lakini hii inategemeana kwani kama Okwi (Emmanuel) ataondoka kwenda nje ya nchi,”alisema kiongozi huyo. 

Aliongeza kwamba uongozi unafanya mazungumzo na klabu mbili zinazomuhitaji Okwi ambapo Kaizer Chief ya Afrika Kusini imefikisha dau la shilingi mi.300 huku  nyingine kutoka nchini Australia imefika shilingi mil.350. 

Aidha kiongozi huyo alisema wamedhaminiria kusajili wachezaji wazuri ambao wataiwezesha timu yao kufanya vema katika michuano mbalimba.li itakayoshiriki wakianza na kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi jijini Dar es Salaam baadaye mwezi huu. 

Simba inayonolewa na Mserbia Milovan Cirkovic, tayari imeshafanya mazungumzo na baadhi ya nyota kutokan nchini Kenya na Uganda ili kuweza kuwasajili katika kikosi chao.

No comments:

Post a Comment