Tuesday, June 5, 2012

SERIE A NEWS: LAZIO YAMTAKA KRASIC


KLABU ya Lazio imetumbukia katika mazungumzao na klabu ya Juventus kwa nia ya kumtaka nyota Milos Krasic.

Taarifa kutoka nchini Italia zimeeleza winga huyo anapendelea kubaki nchini Italia licha ya kwamba Lazio katika usajili wa mwezi Januari walitaka kumsajili. Mserbia huyo (27) hapendelei kuondoka Turin hasa ukizingatia aliipiga chini Offer ya Zenit St. Petersburg. Lazio wameingia katika mazungumzo hayo ya kumtaka Mchezaji huyo wa zamani wa CSKA Moscow baada ya kumtangaza Vladimir Petkovic kuwa Kocha mpya wa Lazio. Lazio inabakiw akuwa klabu pekee ambayo imeonyesha kumtaka nyota huyo. Rais wa Klabu hiyo Claudio Lotito amesema hawezi kukata tamaa bila kupigana  kuwapata wachezaji watakaoweza kuisaidia timu hiyo.

No comments:

Post a Comment