Thursday, June 7, 2012

PIQUE, SHAKIRA WANUNUA JUMBA LA KIFAHARI BARCELONA.



TETESI za kuachana kwa beki wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona Gerard Pigue na rafiki yake wa kike ambaye mwanamuziki nyota wa pop Shakira zimefutika baada ya wawili hao kununua jumba la kifahari ambalo watakuwa wakiishi. Baada ya kutafuta kwa miezi kadhaa hatimaye wawili hao walinunua nyumba hiyo iliyopo kilomita chache kutoka jiji la Barcelona ambayo iko karibu na Uwanja wa Camp Nou pamoja na uwanja wa mazoezi wa klabu ya Barcelona. Suala la kupata nyumba hiyo linaondoa uvumi uliokuwa umesambaa kwa mizei kadhaa kwamba wawili hao walikuwa wametengana huku Pique akilaumiwa kutokana na kutokuwa mwaminifu kwa mpenzi wake huyo. Wawili hao walikutana katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 lilifanyika nchini Afrika Kusini ambapo Shakira alikwenda kutengeneza wimbo wa Waka Waka ambao ulitumika katika michuano hiyo huku Pique akiwa katika kikosi cha Hispania ambacho kilinyakuwa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment