Thursday, June 7, 2012

MCHEZAJI ATAKAYETOKA NJE YA UWANJA KWA AJILI YA UBAGUZI ATAPEWA KADI YA NJANO - PLATINI.


Michel Platini, Rais UEFA.



RAIS wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini amesema kuwa mchezaji yoyote atakayetoka nje ya uwanja wakati wa michuano ya Ulaya kutokana na suala la ubaguzi wa rangi atapewa kadi na mwamuzi. Vyombo vya habari vimekuwa vikigusia mara kwa mara suala la ubaguzi katika michuano ya Ulaya ambayo imeandaliwa kwa pamoja kati ya Poland na Ukraine ambapo hivi karibuni mshambuliaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Italia amesema kuwa atatoka nje kama ataamini anafanyiwa kitendo hicho wakati akicheza. Lakini Platini alionya suala hilo na kudai kuwa mchezaji atayetoka nje ya uwanja atapewa kadi ya njano kwa kujichukulia maamuzi wakati mwamuzi wa mchezo yupo. Platini aliongeza kuwa mwamuzi wa mchezo ndio pekee anaruhusiwa kuchukua maamuzi kama hayo, na anaweza kumaliza mchezo kama kuna tatizo la ubaguzi lililotokea hiyo ndio njia pekee ya kulinda mchezo wa soka dhidi ya ubaguzi.

No comments:

Post a Comment