Wednesday, June 6, 2012

MBEYA UPDATE: TANESCO YATOA OFA KWA WATAKAOFANIKISHA WEZI WA VIFAA VYA KAMPUNI


SHIRIKA la umeme Tanzania (Tanesco) mkoa wa Mbeya limetangaza kuwapatia Sh. 50,000 mpaka Sh. 300,000 wale wote watakaotoa taarifa za uhakika za kufanikisha kuwakamata watu wanaolihujumu shirika hilo.
Neema hiyo imetangazwa jana na Meneja wa Tanesco mkoa wa Mbeya John Bandiye alipokuwa akizungumza ofisini kwake amesema kuwa kumeibuka wimbi kubwa la wezi wa miundombinu ya shirika hilo vikiwemo vyuma, nyaya, umeme na mafuta ya Transfoma ambapo kwa miezi mitatu wezi hao wameiba mafuta katika transfoma 10-13 na kulitia hasara shirika hilo na kuwasababishia usumbufu wananchi.

Amesema kutokana na wizi huo tayari shirika hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuwakamata watu wane ambapo wawili walikamatwa na mafuta ya Trasfoma na wengine wawili walikamatwa na nyaya za umeme ikiwa ni pamoja na wizi wa umeme. Ametoa wito kwa wananchi kuwakamata na kuwahoji wale wote ambao wanawatilia mashaka kuwa si watendaji wa Tanesco hata kama watakuwa wamevaa sare za shirika hilo na kuwapeleka katika vituo vya polisi mpaka watakapothibitishwa na viongozi wa shirika hilo kuwa ni wafanyakazi wake au ni wezi.

Ameongeza kuwa siri za watoa taarifa zitatunzwa na ndiyo maana ameamua kutoa simu yake ili kuwahakikishia wale wote ambao watakuwa na wasiwasi kutoa taarifa kwa watumishi wengine wawasiliane nay eye mwenyewe ikiwa ni pamoja na kufika ofisini kwake.

Transfoma ambazo zimeathirika na wizi wa mafuta ni zenye uwezo wa ujazo wa lita 100-200 ambapo Jiji la Mbeya ndilo limeathirika zaidi na wizi wa mafuta hayo.

No comments:

Post a Comment