Tuesday, June 5, 2012

MBEYA UPDATE: MAMLAKA ZINAZOHUSIKA ZATAKIWA KUSIMAMIA MAZINGIRA KWA NGUVU


Jana ilikuwa siku maalumu ulimwengu ya kuyaenzi mazingira ambapo akali ya nchi zote zilizishiriki katika maadhimisho hayo .

Maadhimisho hayo kitaifa yameadhimishwa mjini Moshi na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.

Wadau mkoani Mbeya wameitaka serikali kuwashughulikia wale wote wanaolima katika vyanzo vya maji na kwenye milima kwa kufanya hivyo.

Mwanaharakati wa Masuala ya Kisiasa na Kijamii mkoani Mbeya Nelson Mwangosi amezitaka mamlaka zinazhusika kusimamia uchafuzi wa mazingira mkoani Mbeya kwani wakazi wa Mkoa wa Mbeya wamefikia kuona kama ni kitu cha kawaida.

No comments:

Post a Comment