Wednesday, June 6, 2012

MBEYA UPDATE: MAITI 10 ZATAMBULIWA AJALI YA INTANGANO


Miili 10 kati ya 13 ya marehemu katika ajali iliyotokea jana(Juni 5) mlima wa Mzalendo nje kidogo ya jiji la Mbeya ikihusisha lori lenye namba T 658 ASJ aina ya FAW lililokuwa na tela lenye namba T 150 ASN lililoigonga Toyota coasta T 188 AWE imetambuliwa.
Taarifa kutoka jeshi la polisi mkoani Mbeya kupitia ofisi za kikosi cha usalama barabarani leo zimeeleza kuwa marehemu watatu bado hawajatambuliwa na kuendelea kutoa wito kwa wakazi mkoani humo kuzidi kujitokeza katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya rufaa kuitambua miili hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,waliotambuliwa ni wanawake Lucia Livingstone(51) mkazi wa katumba wilayani Rungwe,Mwalumu mstaafu Ernesta Kikanga(62) mkazi wa Ifunda mkoani Iringa,Lena Uzuri Ngomano(49) mkazi wa Isongole Rungwe na Bahati Japhari(33) mkazi wa Kyela.

Upande wa wanaume wametambuliwa sita na wote wakiwa wanatokea katika vitongoji vya jijini Mbeya ambao ni pamoja na dereva wa coaster Mwasa Dimond(32) wa CCM Ilomba,Yerusalemu Mwakyusa(35),Emanuel Mwanjanja wa Ilomba,Pius Mbeye wa Uyole,Mwase Piusi wa Iganjo na Mwarine Focus wa Uyole.

Wakati huo huo muuguzi mkuu katika hospitali ya Rufaa dokta Thomas Isdori amesema 13 kati ya majeruhi 20 waliofikishwa wameruhusiwa na kubaki majeruhi saba wanaoendelea vizuri kati yao akiwemo mwanaume mmoja Fodi Mwakabunga(35) mkazi wa Kyela.

Wengine ni wanawake aliowataja kuwa ni Zainabu Bahati(33) mkazi wa Igawilo jijini hapa,Catherine Komba(23) mkazi wa Hatwelo wilayani Mbeya,Neema Mwanarukwa(haijulikani) wa Mlowo Mbozi,Paulina Francis(42) wa Uyole jijini Mbeya,Esther Mgaya (21) na Veronika Chengelo(57) wa mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment