Thursday, June 7, 2012

MBEYA UPDATE: KICHANGA CHATUPWA KWENYE GHUBA YA TAKA MWENGE


Kitoto kichanga chenye jinsia ya kiume kinacho kadiliwa kuwa ni mimba ya miezi kati ya sita (6) na saba (7) kimekutwa kimetupwa katika ghuba la kutupa takataka maeneo ya Shule ya Msingi Mwenge Mwanjelwa, kitoto hicho kimekutwa na msamaria mwema ambaye hakutaka jina lake  litajwe.

Mtu huyo alifika eneo hilo kwa minajiri ya kutaka kutupa takataka aliona kanga iliyoloa damu na aliposogelea akakiona kichanga hicho kikiwa kimewekwa juu ya kanga hiyo na ndipo alipoto taarifa polisi ambao walifika na kukichukua na kuondoka nacho, mpaka sasa haijajulikana ailiye husika na uhalifu huu.

Ukatili huu kwa akina mama umezidi kushamili katika jiji la Mbeya kumekuwa na vitendo vya namna hii vya utupaji watoto  vinajitokeza mara kwa mara ambapo majuma mawili yaliyopita maeneo ya Iyunga kilijitokeza kitendo cha kutupa mtoto katika shimo la maji machafu.  

No comments:

Post a Comment