Tuesday, June 5, 2012

MBEYA UPDATE: BENKI YA POSTA YATOA MSAADA VIFAA HOSPITALI YA META


BENKI ya Posta Tawi la Mbeya imetoa msaada wa Shilingi Milioni 2/= katika Hospitali ya Wazazi Meta Kitengo cha Damu Salamu ikiwa na madhumuni ya kuadhimisha wiki mbili za huduma hiyo hapa nchini ambapo katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini itafikia kilele Juni 14 mwaka huu mjini Songea.
 MENEJA HUMPHREY JULIUS WA BENKI YA POSTA MBEYA
 BENKI YA POSTA TAWI LA MBEYA

 KUNDAELI SARIA AFISA UTUMISHI MPANGO WA DAMU SALAMA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI 

Katika msaada huo Benki ya Posta imetoa vifaa vya kusaidia uchangiaji wa damu salamu ikiwemo T-Shirt zenye maandishi ya kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho hayo ambayo kitaifa yatafanyika Moshi katika benki ya damu salamu ya Hospitali ya KCMC.
Akikabidhi msaada huo Meneja wa Benki ya Posta Mkoa wa Mbeya Humphrey Julius amesema kufuatia changamoto wanazokutana nazo katika kitengo hicho wameona watie mkono wao pia ikiwa ni mwanzo tu wa kusababisha zoezi zima la uchangiaji damu kufanikiwa.

Meneja Humphrey ameongeza kusema Benki ya Posta ni ya Wananchi hivyo ni kazi yao kufanya huduma za kijamii kama ambavyo wamefanya  kwa Kitengo cha Damu salama katika Hospitali ya Meta Jijini Mbeya ili wananchi ama wagonjwa wenye uhitaji wasijepoteza maisha kutokana na upungufu wa damu mwilini. Hata hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ikiwa na madhumuni ya kuwa na akiba ya kutosha ili wagonjwa wanaopatikana na upungufu kusiweko uchache wa damu kwa ajili ya kunusuru maisha yao.

Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Kitendo cha Mpango wa Damu Salama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Kundaeli Saria amesema wanakutana na changamoto nyingi katika Kitengo hicho ambacho ni muhimu wa jamii hivyo ujio wa Benki ya Posta katika kuongeza nguvu ni jambo kla msingi sana. Kundaeli  Saria ameongeza kusema msaada huo ni muhimu sana na kuomba taasisi nyingine kujitokeza kuchangia damu ili kuwemo akiba ya kutosha katika Kitengo hicho adhimu. Hata hivyo aamewataka wananchi kuongeza ushirikiano baina yao ili kuwabaini watumishi wasio waadilifu wanaowatoza kiasi cha fedha kwa ajili ya wagonjwa wao kupewa damu. Kitendo hicho ameekiita ni kukiuka maadili ya kazi  kwani damu hizo haziuzwi. Pia Saria amesema wahitaji wa damu wanatoka katika makundi makubwa mawili ikiwa ni wale majeruhi wa ajali na wenye upungufu wa damu mwili na kwamba isipokuwepo ya kutosha maisha yao huwa matatani. Aidha amewataka wananchi kuondokana na imani potofu kuwa mchangiaji wa damu anapoitoa hujpalia laana kutokana na kwamba damu nyingi itaongezeka kwa kasi na kumleta matatizo hapo baadaye.

Kitaifa itafanyika Moshi ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete na kilele ni Juni 14, 2012

Imeandikwa na Johnson Jabir, Mbeya

No comments:

Post a Comment