Thursday, June 7, 2012

LAVAGNE ABAKIWA NA MIEZI MITANO CAMEROON.


Denis Lavagne.



KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon, Denis Lavagne amepewa mkataba wa mwaka mmoja lakini anaweza kuongezewa kama atafikia makubaliano yaliyowekwa katika mkataba huo. Mkataba huo unsema kocha huyo lazima aiwezeshe timu hiyo ifuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2013 pamoja na ile ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil, pia lazima aipandishe timu hiyo katika orodha ya viwango vya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA katika nafasi ya timu 20 bora. Akiusoma mkataba huo, Waziri wa Michezo wa nchi hiyo amesema kuwa mkataba wa kocha huyo unaanzia Novemba mosi mwaka 2011 na kuishia Octoba 31 mwaka 2012 ikimaanisha kuwa Lavagne amebakiwa na miezi mitano tu ya kuwashawishi wamuongeze mkabata mwingine au aondoke zake. Pamoja na kwamba mshahara atakaopewa kocha huyo haukuwekwa wazi lakini kuna tetesi kuwa Lavagne atakuwa akilipwa dola 20,000 kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment