Tuesday, June 5, 2012

GLOBAL NEWS: WASHIA WA YEMEN KUSHIRIKI MAZUNGUMZO


Waislamu wa madhehebu ya washia wanaolidhibiti eneo kubwa la Kaskazini mwa Yemen watashiriki katika mazungumzo yanayolenga kuutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa nchini humo.

Tangazo hilo limetolewa na afisa anayehusika na maandalizi ya mazungumzo hayo. Awali waasi wa Houthi walikataa kushiriki mazungumzo hayo ya kitaifa ambayo ni sehemu ya makubaliano ya mpito yaliyoungwa mkono na Saudi Arabia na Marekani na yaliyomuondoa madarakani rais wa muda mrefu  nchini Yemen, Ali Abdullah Saleh, mwaka huu. Marekani na Saudi Arabia zinataka kuona mpango huo ukileta amani na usalama katika taifa hilo masikini ambalo wanajeshi wake wako katika mapambano dhidi ya makundi ya wanamgambo yanayofungamanishwa na mtandao wa Al-Qaeda.     

No comments:

Post a Comment