Wednesday, June 6, 2012

GLOBAL N EWS: AHMADINEJAD ALAANI SIASA CHAFU ZA MAREKANI


Akihutubia wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Peking katika mji mkuu wa China, Beijing, Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa 'mbwa mwitu huyu (Marekani) ameeneza vita katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa kushirikiana na Wazayuni na kulikandamiza na kulidhulumu taifa la Palestina.'

Rais wa Iran amesema, jana dunia inahitaji viongozi wanaochaguliwa na wananchi na wanaozingatia maadili mema.Rais Ahmadinejad aliwasili China Jumanne jioni akiongoza ujumbe wa ngazi za juu kwa lengo la kushiriki katika kikao cha 12 cha viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Akiweko mjini Beijing, Ahmadinejad anatazamiwa kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa China.

No comments:

Post a Comment