Tuesday, June 5, 2012

FIFA YAONYA UKUAJI WA MATUMIZI YA DAWA ZA KUPUNGUZI MATUMIZI KWA WACHEZAJI.


Dr. Jiri Dvorak.



OFISA mkuu wa afya wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Dr Jiri Dvorak amesema kuwa matumizi ya kupindukia ya dawa za kutuliza maumivu inahatarisha soka la wachezaji wengi wa kimataifa. Katika uchunguzi wake daktari huyo amesema kuwa asilimia 40 ya wachezaji walioshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 walikuwa wakitumia dawa karibu katika kila mchezo waliocheza. Kuelekea katika michuano ya Ulaya inayotarajiwa kuanza siku chache zijazo Dr Dvorak amesema kuwa kuna umuhimu wa FIFA kuliangalia tatizo hilo upya kabla halijaleta madhara zaidi kwa wachezaji kwa siku zijazo. Daktari huyo aliendelea kusema kuwa wachezaji wenye umri mdogo wamekuwa wakiwaiga wachezaji wenye umri mkubwa kwa kutumia vidonge vya kutuliza maumivu kila mara. Mshambuliaji wa kimataifa wa Croatia na klabu ya Bolton Wanderers ya Uingereza Ivan Klasnic ndiye anakuwa mchezaji wa kwanza dunia kurejea kucheza tena soka baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza figo. Mchezaji huyo alifanyiwa upasuaji huo wakati akiwa anacheza Werder Bremen ya Ujerumani mwaka 2007 ambapo anawalaumu madaktari wa timu hiyo kwa kushindwa kugundua tatizo lake haraka na kuwa wanampa vidonge vya kutuliza maumivu kwa kipindi kirefu.

No comments:

Post a Comment