Monday, June 11, 2012

EYEW APEWA TUZO GHANA.

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini Ghana kimempa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka 2011 kiungo wa kimataifa wa nchi hiyo anayecheza katika klabu ya Marseille ya Ufaransa Andre Ayew. Ayew ambaye pia mapema mwaka huu alinyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBC alinyakuwa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji wenzake Emmanuel Agyemang-Badu na Harrison Afful katika kinyang’anyiro hicho. Sherehe za tuzo hizo zilifanyika Jumamosi usiku jijini Accra nchini humo ambapo kwa mujibu waratibu wa tuzo hizo, Ayew ameonyesha kiwango kikubwa katika timu yake ya taifa na klabu kwenye msimu wa mwaka 2010/2012 ndio maana amepewa tuzo hiyo. Hatahivyo tuzo ya jumla ya mwanamichezo bora wa mwaka imechukuliwa na mshindi mara mbili wa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya riadha kwa watu wenye ulemavu maarufu kama Paralimpic, Ajara Mohammed.

No comments:

Post a Comment