Wednesday, June 6, 2012

EURO 2012: UKRAINE, ENGLAND NA FRANCE ZAWA ZA MWISHO KUWASILI KATIKA MICHUANO HIYO.

TIMU ya taifa ya Ukraine ambao ni wenyeji wenza wa michuano ya Ulaya kwa mwaka huu imekuwa timu ya mwisho kuwasili kwa ajili ya michuano hiyo ikitokea nchini Austria ambapo walikuwa wameweka kambi. Mshambuliaji mkongwe wa timu hiyo Andriy Shevchenko na wachezaji wenzake walipokelewa kwa tafrija fupi ya kimila katika Uwanja wa Ndege ulipo jijini Kiev kabla ya kuelekea katika hoteli waliyofikia. Ukraine imerejea nyumbani huku ikiwa na maumivu ya kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Uturuki katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu ambapo wanatarajiwa kuweka kambi yao katika uwanja wa mazoezi wa timu ya Dynamo Kiev. Timu zingine ambazo pia zimewasili leo ni pamoja na Sweden, Uingereza na Ufaransa ambapo michuano hiyo itakayofanyika katika mataifa mawili ya Ukraine na Poland inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 8 mpaka Julai 1 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment