Tuesday, June 5, 2012

EPL NEWS: SHINJI KAGAWA KUTUA OT


KLABU ya Manchester United, hatimaye imemsajili kiungo wa Borussia Dortmund, Shinji Kagawa kwa dau ambalo halijawekwa wazi na sasa kilichobaki ni mchezaji huyo kufanyiwa vipo na kupewa kibali cha kufanya kazi Uinegereza, mambo ambayo haina shaka yatakwenda sawa kwa nyota huyo aliyeichezea Japan mechi 30.

Tangu ajiunge na Dortmund kwa dau la pauni 285,000 akitokea Cerezo Osaka mwaka 2010, Kagawa ameisaidia Dortmund kutwaa mataji mawili mfululizo ya Bundesliga, akifunga mabao 29 katika mechi 71. Kagawa alikuwa majeruhi wakati wa Kombe la Mataifa ya Asia mwaka jana, ambayo yalimuweka nje ya Uwanja katika mzunguko wa pili wa msimu wake wa kwanza Ujerumani.

Pamoja na hayo, nyota huyo wa Japan, alifungia mabao manane katika mechi 18 katika msimu huo wa ligi na akatajwa kwenye kikosi cha msimu cha Bundesliga.
Msimu huu, ameiwezesha pia Dortmund kutwaa taji la DFB-Pokal kwa mara ya tatu katika historia ya klabu hiyo. Lakini kukosekana kwenye kikosi cha Japan katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010, kuna uwezekano Manchester United italazimika kukata rufaa ili apatiwe kibali cha kufanya kazi Uingereza.
Kwa sasa, Kagawa anakosa vigezo vya moja kwa moja vya England, kuwa ameitumikia timu yake ya taifa kwa asilimia 75 katika miaka miwili iliyopita, aingawa hadhi yake kuwa mshindi wa mataji mawili ya Bundesliga itamfungulia milango ya kukipiga Old Trafford.

Manchester United is delighted to announce that it has agreed terms with both Borussia Dortmund and Shinji Kagawa for his transfer to the Club.
The deal is subject only to the player medical and obtaining a UK work permit. These conditions are anticipated to be completed by the end of June.
Further details will be announced in due course.

No comments:

Post a Comment