Tuesday, June 5, 2012

DROGBA KUGOMBANIA KIATU CHA DHAHABU.



NAHODHA wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba ni miongoni mwa wachezaji waliopo katika orodha ya kugombania tuzo ya kiatu cha dhahabu ambayo kwasasa inashikiliwa na kiungo wa Manchester United Ryan Giggs aliyekabidhiwa tuzo hiyo Octoba mwaka jana jijini Monaco. Tuzo hiyo ambayo ilizinduliwa na Mfalme wa Monaco mwaka 2003, ni ambayo anapewa mchezaji aliyepata mafanikio katika soka kwa kipindi kirefu cha uchezaji wake ambaye anakiwa kuwa na umri unaofikia miaka 29 na kuendelea. Mbali na Drogba wachezaji wengine walioteuliwa kugombea tuzo hiyo safari hii ni pamoja na Gianluigi Buffon, Iker Casillas, Zlatan Ibrahimovic, Kaka, Andrea Pirlo, Carles Puyol, Raul, Clarence Seedorf na Xavi Hernandez ambapo mshindi atapatikana kwa kura zitakazopigwa katika mtandao. Wachezaji ambao wameshawahi kunyakuwa tuzo hizo toka zilivyoanzishwa na miaka yao ni pamoja na Roberto Baggio-2003, Pavel Nedved-2004, Andriy Shevchenko-2005, Ronaldo de Lima-2006, Alessandro Del Piero-2007, Roberto Carlos-2008, Ronaldinho-2009, Francesco Totti-2010 na Ryan Giggs-2011.

No comments:

Post a Comment